Nakala hii inapatikana pia kwa Kiingereza.
Je, teknolojia yenye umri wa miaka 140 inaweza kuwasaidia wakulima wa Kenya kuwa na fanaka zaidi? Miaka michache iliyopita, Sidai Africa, biashara inayothamini miingiliano ya watu iliyo Nairobi, iliamini kuwa jibu ni “ndiyo” thabiti.
Chanjo ya kwanza ya mifugo iliundwa Ufaransa mwaka wa 1879. Teknolojia yenyewe haikuwa kitu kipya, lakini Sidai iliamini kuwa iwapo wakulima zaidi wangekuwa wanaweza kufikia chanjo za mifugo, lingekuwa jambo linalobadilisha hali kabisa. Mawazo yao yalivutia Bill & Melinda Gates Foundation.
Wakati Bill na Melinda Gates walipoanza kutoa misaada zaidi ya miaka 20 iliyopita, eneo moja waliloangazia ni afya. Walikuwa wamesoma habari kuhusu jinsi mamia ya maelfu ya watoto walivyokuwa wanakufa kutokana na magonjwa yanayoweza kukingwa kwa sababu hawangepata madawa na chanjo walizohitaji.
Walipo fanya utafiti, walitambua kuwa utapiamlo pia ulikuwa unawazuia milioni ya watoto kukua na afya nzuri. Watoto walihitaji vyakula vyenye virutubishi zaidi na mara nyingi lishe hiyo ilipatikana kupitia kwa kilimo. Hapo ndipo Bill na Melinda walipoanza kuuliza, “Wakulima wangewezaje kukuza mifugo yenye afya na mimea inayotoa mazao mengi ili kufanikiwa na kukimu familia zao zaidi?”
Maswali haya ni muhimu hasa kwa Kenya, ambapo kilimo kinachangia takribani theluthi ya uchumi mzima, na kuna uwezo mkubwa ambao hautumiwi. Kadiri ya robo ya mifugo yote nchini Kenya hufa kila mwaka kutokana na magonjwa yanayoweza kukingwa. Mazao ya mimea nchini Kenya mara nyingi yamekuwa theluti moja—au chini—ya yale ya nchi zingine. Sidai iliona nafasi ya kuboresha hali. Walikuwa na mawazo na kuyaleta kwa Gates Foundation, ambayo ilikubalikutoa pesa ili kugeuza mawazo hayo kuwa uhalisia.

Ufadhili wa awali umeiruhusu Sidai kuwasaidia zaidi ya wakulima 450, 000 wa Kenya. Wametoa chanjo kwa milioni ya mifugo na wanauza malisho yao bora na mbegu katika maelfu ya maduka. Wanatoa huduma za tiba ya mifugo na wameunda mfumo wa teknolojia mpya. Wafanyakazi waliofunzwa na Sidai husafiri kwa pikipiki ili kuwasilisha maarifa na huduma kwa mashamba madogo mashinani. Wanatoa huduma za kupima udongo ili wakulima wajue ni mbolea zipi hasa zitakuwa bora zaidi.
Hii ndiyo sababu inayoifanya Gates Foundation kufadhili miradi ya kilimo nchini Kenya: kuhakikisha kuwa wakulima wana zana zote wanazohitaji ili kulisha familia zao na kuchuma mapato mazuri.
Sidai ni shirika moja tu linalofanya kazi hii. Gates Foundation hushirikiana na mengine zaidi ambayo lengo lao ni kuwasaidia wakulima, ikiwemo International Livestock Research Institute huko Nairobi na Alliance for a Green Revolution in Africa. Gates Foundation hufadhili orodha ndefu ya miradi Kenya, ikiwemo mikopo kwa maelfu ya wakulima wadogo; utafiti kuhusu jinsi ya kupambana na tauni ya kondoo na mbuzi; na kuunda mbegu zinazostahimili kiangazi na joto, ili wakulima wa Kenya waweze kufanya mabadiliko ili kulingana na hali ya hewa ya dunia inayobadilika.
Hivi ndivyo mapinduzi ya kilimo hufanyika katika nchi: hayaji kutoka nje; huanza katika eneo husika—au katika kesi hii, ndani ya ardhi ya eneo husika. Wakulima wadogo hushirikiana na mashirika ya ndani kama Sidai ili kutambua changamoto zao na kuunda suluhisho. Wakati huo huo, mashirika kama Gates Foundation husikiliza na kujifunza: kisha yanaweza kuingilia kati kwa ufadhili na ushauri. Mwishowe, mazao huwa yenye afya, na watoto pia.
Masasisho katika tovuti yetu
Asante kwa kutembelea ukurasa huu. Sehemu kubwa ya tovuti yetu ipo kwa Kiingereza pekee kwa sasa. Tunaendelea na mchakato wa kusasisha maudhui yetu ili kutoa lugha nyingine.
Kuhusu Gates Foundation
Kwa kuongozwa na imani kuwa kila maisha yana thamani sawa, Bill & Melinda Gates Foundation hufanya kazi ili kuwasaidia watu wote kuishi maisha yenye afya na fanifu. Katika nchi zinazostawi, ingalenga kuboresha afya ya watu na kuwapa fursa ya kujiondoa kwenye njaa na umaskini uliokithiri. Ndani ya Marekani, inanuia kuhakikisha kuwa watu wote—hasa wale walio na rasilimali chache zaidi—wanafikia nafasi wanazohitaji ili kufanikiwa shuleni na katika maisha. Ukiwa na makao ndani ya Seattle, Washington, na ofisi kote duniani, wakfu huu unaongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Mark Suzman, chini ya uelekezi wa Bill na Melinda Gates na Warren Buffett.
Published 1/6/21



